Galaxy of Thoughts

Mental journies shuttling between utopia, dystopia and bordering paranoia.

22 Oct 2020

Ningependa kukupa

Ningependa kukupa Mercedes lakini bado sijapata Bahati

Ningependa uone ndani ya Audi lakini ni kama Jesus ni wa Kabi, itabidii nimetafuta wangu

Ningependa tuende holiday ingine more fire but Bonfire hawanijui na Kabu hanitambui na first name basis

Ningependa tuoneshane mapenzi yetu tele kwa Telly but wacha kwanza tukeep up with the Muraya’s

Ningependa kukupenda kwa matendo na zawadi kama navyo ona wengine wakifanya, lakini kwa sasa hakikisho langu ni kwamba mapenzi niko nayo kwako ni ya thati

Ningependa kuandikia nyimbo na jina la nyimbo liwe lako, lakini niliambiwa sauti yangu haiwezi toa nyoka pangoni, labda kitu inaweza fanya ni kutishia watoto wadogo mtaani watoroke hapa Pangani

Mawazo yangu nimakuu lakini bado vitendo ni vitendawili

Yale nimekufanyia ni duni yaweza fananishwa na za wahuni

Jana ulinipa block kwa vile sikutuma fare lakini I swear fuliza walikuwa wamenifukuza, Mshwari waliniblue tick last year mambo si shwari

Uwezo wangu bado tu iko kwa ndoto, inaniwasha kwenye koo kama moto

Ni mimi wako mpenzi bila hela ila natumai unanielewa, Msani bila sanaa